Nahreel Alinitengenezea Hit Yangu ya Kwanza Afrika, Siwezi Kuacha Kufanya Naye kazi – Jux

Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa wakifanya kazi na Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The Industry baada ya kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.

Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni mshkaji wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua kubadilisha ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.

“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You, naweza kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,” Jux ameimbia Bongo5.

“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi kuwasema sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda nisingepata kitu tofauti,” amesisitiza.

Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China na pia Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.

“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya naye kazi pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi haijaniathiri chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka kufanya, kwahiyo mimi naona ni sawa. Kwanza mimi ni mmoja wa watu niliyeona hivyo yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia kwasababu alikuwa anafanya kazi sana.”

Wiki iliyopita Jux aliachia wimbo wake mpya, Wivu aliorekodi kwenye studio za AM Records.