Lulu Afunguka Adai Hajawahi kutoka Kimapenzi na Ali Kiba

Msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha tetesi ya muda mrefu ya kutoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Aje’ Ali Kiba.
Muigizaji huyo mahiri wa filamu amekiambia kipindi cha Weekend Chart Show cha Clouds TV kuwa hajawahi kutoka kimapenzi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ali Kiba kwa muda wowote, sijawahi,” alisema Lulu. “Na hatujawai kuwa na ukaribu wa namna hiyo, lakini ni watu ambao we known each others, na tukikutana tuongea na mambo mengine,”

Hata hivyo kwa sasa muigizaji huyo anadaiwa kutoka kimapenzi na CEO wa EFM, Majay kutokana na wawili hao kuwa karibu zaidi katika kipindi hiki.