Idris Sultan aanza kutoza pesa kwa wanaotaka KIKI kutoka kwake

Kiki ndio kila kitu hapa mjini, wasanii na watu wengi hapa Bongo wamekua maarufu kutokana na Kiki au Skendo zinazosambazwa kuwahusu wao. Wapo waliofanikiwa hadi maisha yao kua mazuri kutokana na kiki au skendo wanazojizushia ili wajulikane na watu.
Sasa kutokana na watu kuhitaji kiki basi Idriss Sultan ambae kwa sasa anatoka na Wema amenzisha kitu kinaitwa KikiPesa. Yani kama unahitaji kiki kutoka kwake lazma umlipe kwani kupitia yeye unaweza kupata pesa au umaarufu kupitia jina lake. Unaweza mskiliza mwenyewe akielezea huduma yake hiyo mpya hapa kwenye video...