Hamisa Mobeto: Bado Kuna Watu Wanadhani mtu Kuwa Model ni Uhuni
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amewataka wazazi kuuwaacha watoto kike/wakiume waingie kwenye fashion na kuachana na dhana ya kwamba kufanya modeling ni uhuni.
Mobeto

Akiongea na Bongo5 wiki hii wakati akitoa maoni yake juu ya nini kifanyike ili kuboresha tasnia ya mitindo, Hamisa amewataka wazazi kuichukulia tasnia ya fashion kama sector nyingine za ajira.

“Unajua Watanzania wengi bado hawajajua nini maana ya modeling , wengine wanadhani ni uchafu, uhuni,” alisema Mobeto. “Tanzania kuna Wanawake wazuri sana, kama wazazi wakiwaruhusu vijana wao kufanya modeling basi Tanzania tutafika mbali sana kwa sababu tuna warembo wengi sana,”

Pia mrembo huyo ameitaka serikali kuangalia tasnia ya fashion ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana wengi pamoja na kuitangaza nchi.