Fella: Mwanamuziki Ruby Ana ‘stress’ Ndio Maana Hajaonekana Kwenye Video Yamoto Band

Ruby alikuwa ana ‘stress’ ndio maana alishindwa kutokea kwenye video ya wimbo SU wa Yamoto Band alioshirikishwa.

Meneja wa kundi hilo, Said Fella amekiambia kipindi cha E News cha EATV kuwa hiyo ndio sababu aliyokuwa akipewa na Ruby. Amedai kuwa baada ya kuona kuwa Ruby amekuwa akitoa sababu hiyo kwa muda na hawakutaka asishiriki akiwa hana mood, walilazimika kuifanya bila yeye.

Kwenye video hiyo anaonekana msichana mwingine akiimba sehemu ya Ruby.

Haijafahamika mara moja ni mambo gani yanamsibu muimbaji huyo kiasi cha kumpa msongo wa mawazo lakini kwa wanaofahamu, stress ni kitu kinachoweza kukuondelea mood ya kufanya vitu vingi.

Bongo5