EXCLUSIVE   One the Incredible Ft. Sampamba – Ndotoni (Lyrics) - MISTARI

One the Incredible – Ndotoni (Lyrics)

[Verse 1 – One Incredible]
 
Mimi ndo…
Peasant nephew nilietekwa na master’s niece
Mapenzi sanaa yake ni masterpiece
Ameniteka mjanja nikatangaza peace
Na siezi toroka hata nikiwa na master key
Sasa miss utanikosha ama ndo juu juu?
Mchezo mi ni kocha, uchezaji nimeshafuzu
Niwe zuzu ama chizi
Mchizi nitazama pale pote unataka nipige mbizi, sasa…
Niruhusu nikuhusu nikupe true love
Kuku nitanunua kwa mganga uende kwa ruksa
Ningekuwa na vyote mi vyote ningeshakupa
Niokote, niongoze, nisiote giza kunapokucha
Wangu miss independent, uishi nikupende
Unipende pia ili isiwe rahisi nikutenge
We wa pekee, wangu mwema nasema
Naomba uwe wimbo wangu nikuimbe tena na tena

[Chorus – Sampamba]

Nikiwa ndotoni, naota kama nipo na we
Nikiamka sikuoni, I wish nikupate we
Najua mi ni msela sana, nikubali mama
Nifanye niwe na furaha
Tena nitajituma sana, usiku, mchana
Mpenzi usilale njaa

[Verse 2 – One Incredible]

Ningependa niwe yule unaemtaka, unaempenda, unaemjua
Yule aliyekuondoa mashaka aliyekuacha alipozingua
Niwe dira yako unapotaka safiri kifikra
Nitakupeleka mpaka mahala hujawahi fika
Hujawahi shikwa ka gita la kiispanyora
Nikapiga chord nitoe ala hijawahi sikika
Kweli unapotesha, uko beautiful na uko sexy
So shori we ni definition ya fly sister
Una smile ya pekee, dimpo za kuficha
Bad girl, shawty wa ku-rock jeans na sneakers
Apple body and booty, cute wa kiafrika
Nakuhitaji zaidi ya mshiko kwa bitozi mwenye sifa
Uko F-L-Y, X-L thighs
Ni sumu mpaka kwa mbu kama X-pel
Hi, naitwa Ali, machizi wananiita One
So habari mrembo? Ningefurahi kukufahamu

[Chorus – Sampamba]


Nikiwa ndotoni, naota kama nipo na we
Nikiamka sikuoni, I wish nikupate we
Najua mi ni msela sana, nikubali mama
Nifanye niwe na furaha
Tena nitajituma sana, usiku, mchana
Mpenzi usilale njaa

[Verse 3 – One Incredible]


Mi napenda uko simple, fresh
Dimple kwenye face
Ni zaidi mwanamitindo yako maringo na shape
Nataka nikupe habari kama jingle kwa gazeti
Wanakuita CD, kwangu wimbo wa cassette
Mtoto fimbo ya staff, huendi chimbo kwa madenti
Nipe love hata kidogo kama mchinjo wa bajeti
Niko single shori, kimtindo niwe the next
Niko online, acha maringo binti connect
Usikubali kukataa, usikatae kukubali
Fanya iwe nae nae ili baadae iwe shwari
Wanasema na rhyme kali
Ila hizi conversation huwaga ma-night kali
Nikikupata nitaimba kama Ben
Na nikikukosa nitatunga wimbo ka wa Ben Pol
Acha mapozi ili dada akuite wifi
Mama akuite mkwe, na kaka akuite shemzo

[Chorus – Sampamba] x2


Nikiwa ndotoni, naota kama nipo na we
Nikiamka sikuoni, I wish nikupate we
Najua mi ni msela sana, nikubali mama
Nifanye niwe na furaha
Tena nitajituma sana, usiku, mchana
Mpenzi usilale njaa