Mercato : Mchezaji umoja mahiri wa Barcelona anaonekana kuondoka
Vyombo vya habari za Italia na Hispania, zinawaka kwa habari ambazo zinaonesha kuwa beki mahiri wa Argentina Javier Mascherano (31) wa   FC Barcelona  amekwisha kubaliana na klabu moja ya Italia nayo si nyingine ni Juventus.
Hakika, gazeti la Ad Sky Sport Italia, imefichuwa habari kuwa viongozi wa mchezaji wamekuwa na maongezi kuusu uwezekano wa kumsajili beki uyo katika klabu ya Italia, tayari mchezaji amefikia kukubali  kujiunga na klabu hio kwajili ya msimu ujao.
Mchezaji wa Albiceleste ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Juni 2018, ameridhika kujiunga na wa bingwa wa Italia na kuongezwa mshahara wa juu sana kuliko mshahara wake wa milioni nne kwa mwaka katika klabu ya barcelona na ukilinganisha na kazi kubwa anayo changia katika klabu hio.
Kocha Massimiliano Allegri, amevutiwa na beki uyo ila upande mwingine wa barcelona wameonekana kama hawana nia ya kuachana na mchezaji hata umoja ambaye amechangia ufanisi wa Ubingwa wa Hispania. habari hii itaendelea