EXCLUSIVE  Harmonize - Penzi Ft. Raymond (Lyrics) Mistari

Harmonize - Penzi Ft. Raymond (Lyrics)
[Verse 1]
[Raymond]
Nawaza kwanini sikumjuaga zamani
(Oh mama)
Pendo lake zito mpaka lavunja mizani
(Oh mama)
Yeye na mimi kachoo nisharuka nyie
(Oh mama)
Wasojua mapenzi pole jamani
Eti alikuwa bachelor, aibu gani!

[Harmonize]
Aliyeumba dunia
Akayaumba na mapenzi
Wala hakukosea
Ila mwenzenu mi siwezi
Nilishapenda
Ila nkatendwa
Moyo ulidunda, masikini roho
Mbona nlikonda
Licha ya kuhonga
Kuweka vibanda
Nishaomba poo
Mwenzangu bado hujajua
Baki unicheke
Kwako yamechanua
Ngoja yanyauke
[Raymond]
Andazi si kitumbua, acha mapepe
Ukipendwa tanua, kwanini nsideke?
[Chorus x2]
[Raymond]
Jamani nimependa mi, nimependa mi
Nimependa mi, nataka nimuweke ndani
[Harmonize]
Mwenzako nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mie, mapenzi siyatamani
[Verse 2]
[Raymond]
Ana mapenzi ya bara kachanganya na pwani
Vipi nitajinasua?
Rangi kama chotara, shape sio mjapani
Marashi huzibi pua
Ameumbika sina budi nisifie
Akipika natamani nilipie
Sehemu ya upanga uliweka kiwembe
Ndo maana Mwasi akaona ajichenge
[Harmonize]
Kwa wenzako sikia, sikia mwana
Ila kwako utalia, utalia sana
Mi nilikuwaga fundi, fundi zaidi yako
Power ka milundi, nikiganda kama sumako
Na kutia pesa madegeje, asiniache
Nikamchanganya akolee, asiwake
Penzi upepo wa bahari, mara kusi shwari
Yaki-change hatari, na usiombe
[Chorus x2]
[Raymond]
Jamani nimependa mi, nimependa mi
Nimependa mi, nataka nimuweke ndani
[Harmonize]
Mwenzako nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mie, mapenzi siyatamani
Nimetendwa eh
Mwenzenu ninatendwa
Nimetendwa
[Outro]
[Raymond]
Nimependa mi, nimependa mi
Nimependa mi, nimependa mi
[Harmonize]
Nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mie, nimetendwa mie


Download: Harmonize - Penzi Ft. Raymond