Mfahamu Gigy Money Kwa Ufupi | Gigy Money Biography

      Gift Stanford a.k.a Gigy Money, amezaliwa Tanzania mkoa wa Dar Es salaam wilaya ya temeke mnamo mwaka 1998 mwezi julai tarehe  18 (kumi na nane).Gigy amemaliza elimu yake ya msingi Mivinjeni,na kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Keko.
Gigy ni mtoto wa pili katika familia ya mzee Stanford. Gigy ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flavour),Mwanamitindo mwenye kuonekana kwenye video za wasanii wa hip hop na wengineo (Video Vixen),vile vile ni Muigizaji (Actress).

Baadhi ya kazi alizokwishazitengeneza ni pamoja na , Majojorijo , Alela , Na SUPU.Baadhi ya Videos za wasanii wengine ambazo tayari mwanadada huyo ameshashiriki kama Video Vixen ni pamoja na I get High ya God Zilla,Shika Adabu yako by Ney Wa Mitego,na nyingine nyingi.

Gigy
Amewahi kufanya kufanya kazi katika kituo cha East Africa Television (EATV),Kituo hicho kupitia kipindi cha Friday Night LIVE alikua akilipwa kwa kila show inayoruka hewani siku ya ijumaa.


Video: Mahojiano ya Gigy Money na Global TV Online