YouTube Waja na Teknolojia Mpya ya 360

CHANELI maarufu ya Video, YouTube kwa kushirikiana na rapa maarufu duniani kutoka nchini Marekani, Snoop Dogg jana ilizindua mfumo mpya wa kiteknolojia ya 360 uitwaoSnoopavision utakaosaidia kuboresha utazamaji wa video mtandaoni.

Katika mfumo huo wa kiteknolojia, mtazamaji pindi atakapofungua video yeyote ya YouTube ataona icon ya Snoopvasion kwa chini, akiibofya itafungua video yenye maelekezo namna ambavyo inafanya kazi.
Meneja wa Ubunifu wa YouTube, Ben Relles aeelezea kuwa teknolojia hiyo ya 360 imewafanya wapige hatua katika nyanja ya kusaidia watazamaji wao wa video. Teknolojia hii itakuwa maalum kwa video zilizopigwa kwa kutumia drones.
Kwa upande wake rapa Snoop Dogg amesema kuwa, tofauti na zamani ambapo video ilionekana pembe moja kwa mbele pekee (front focusing), lakini kwa teknolojia hii mpya mtu ataweza kuona video kwa mzunguko wa nyuzi 360 za duara. Mtazamaji akitaka kuona mbele, nyuma, juu, chini au pembeni akitumia kifaa chake kama kompyuta, ipad au smart phone yake atabofya icon ya kuzungusha (ipo kama duara) iliyopo upande wa kushoto juu kwenye video hiyo.