Ndanda Kosovo Afariki Dunia
Ndanda Kosovo enzi za uhai wake.
MWIMBAJI nguli wa Muziki wa Dansi hapa nchini kutokea Kongo, Ndanda Kosovo amefariki dunia leo Jumamosi asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa kwa maradhi ya  tumbo.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mmoja wa Viongozi wa Wanamuziki wa Kongo chini Tanzania, King Dodoo amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa Ndandaa kosovo alifikishwa Hospitali ya Mwananyamala juzi na kulazwa tatizo la maradhi ya tumbo.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, jana alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako mauti yamemkuta leo asubuhi.
Ndanda Kosovo aliwahi kutamba na Bendi ya Wajelajela Original miaka ya 2000 na atakumbukwa kwa nyimbo kama, Jela, Chini Ya Uunzi, Chozi La Mnyonge na nyingine nyingi.
“NDANDAA KOSOVO APUMZIKE KWA AMANI!”