Dkt. Shein Atangaza Baraza Lake la Mawaziri

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa.
Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.
Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.
2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.
3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.
4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohd Aboud.
5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohd.
6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.
7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.
8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.
9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.
10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.
11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohd.
12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.
13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.